} LUCY PATRICK WATZ: YALIYOJIRI KATIKA JUMBA LA BIG BROTHER.

YALIYOJIRI KATIKA JUMBA LA BIG BROTHER.


SHINDANO la Big Brother Afrika linalofanyika nchini Afrika Kusini ambalo limeshirikisha nchi zipatazo 14 kutoka barani humo limeanza kushika kasi katika siku yake ya nne toka lizinduliwe rasmi Jumapili iliyopita. Washiriki wapatao 28 kutoka nchi hizo waliingia kwenye jumba hilo ambalo watakaa kwa siku 91 huku Tanzania ikiwakilishwa na washiriki wawili Feza Kessy ambaye aliwahi kuwa Miss dar Indian Oceans na Miss Ilala mwaka 2005 na Amy Nando ambaye ni mwanafunzi. 
Katika shindano la safari hii ambalo washiriki wamegawanywa katika majumba mawili tofauti ambalo yamepewa jina moja likiitwa Jumba la Dhahabu(Diamond) na Jumba la Rubi (Ruby) huku washiriki wa Tanzania wote wawili wakiangukia jumba la dhahabu. Wiki hii BIG BROTHER amewapa kazi washiriki wote katika majumba mawili haswa wanaume kuwafundisha jinsi ya kutongoza wanawake, vitu gani huwa vinawavutia na wanaume wa aina gani wanawake hupendelea. Katika zoezi hilo ambalo kila mwanaume amekabidhiwa mwanamke wa kumtongoza, wanawake watakachotakiwa kufanya wao ni kutoa alama kwa mwanaume ambaye wanamuona ndiye aliyefanya vizuri zaidi katika zoezi na alama hizo zinaanzia 10.


NANDO: 
Zoezi walilopewa mapema jana na Biggies limeonyesha kuwaingia baadhi ya washiriki kwa kuondoa mipaka ya kuogopana kati mwanamke na mwanume baada ya mshiriki wa kiume wa Tanzania Nando kuonyesha ukaribu na ukaribu na mshiriki wa mrembo kutoka Zambia aitwaye Dillish. Wawili hao walionekana kuwa pamoja kwa kipindi kirefu na baada kwenda pamoja bafuni na kuingia katika beseni la kuogea (Bath Tub) huku wakiwa katika mazungumzo ya hapa na pale.

Je mahusiano hayo yanaweza kugeuka na mapenzi?
Kwa upande mwingine mshiriki wa Ghana Elikem ameonyesha tabia za kupenda kurukaruka na wanawake baada ya muda wa kulala jana usiku kutoka katika kitanda cha mshriki wa Tanzania Feza na kukimbilia kwenye kitanda cha mshiriki wa Malawi Fatima na kujifunika shuka huku wakionekana kuzungumza kwa kunong’ona. Wiki hii watanzania wote wawili Nando na Feza wako salama huku washiriki ambao wako katika hatari ya kutoka ni Denzel wa Uganda, Betty wa Ethiopia, Hudda wa Kenya, Selly wa Ghana na Natasha wa Malawi.

0 comments: