} LUCY PATRICK WATZ: WEMA SEPETU ANYOA NYWELE ZAKE. PIA ASEMA NI KWELI ANAKUJA NA REALITY TV SHOW.

WEMA SEPETU ANYOA NYWELE ZAKE. PIA ASEMA NI KWELI ANAKUJA NA REALITY TV SHOW.WEMA SEPETU AVAA GAUNI LA MIL.1.5 KUTOKA KWA MBUNIFU WA KITANZANIA

Actress Wema Sepetu anadaiwa kuvaa gauni la thamani ya shilingi milioni 1.5 katika event ya Women Celebration iliyoandaliwa na Shamimu Mwasha wa 8020 Fashions. Gauni hilo lililomtoa vizuri Wema kiasi cha kuonekana kama mwana wa mfalme lilidizainiwa na talented Tanzanian designer Eve Collection ambaye nguo zake zimekuwa zikimtukuza mwanamke wa kisasa wa kiafrika kwa kuchanganya African and western touches. Eve Collection pia imeshavalisha mastaa kadhaa kama Madam Rita.
Kama ni kweli basi ni lazima Wema apongezwe kwa moyo wake wa kizalendo na fikra positive kwa kuthamini na kuona kuwa hata wabunifu wetu wana uwezo wa kutengeneza nguo yenye ubora kama za designers wakubwa wa nje, hii ni kwa sababu mastaa wengi wananunua viwalo kutoka nje hata visivyo na ubora wakati wapo designers wa Tanzania wenye vipaji na kazi nzuri. Gharama ya gauni hilo iliandikwa na meneja wa Wema aitwaye Martin Kadinda katika blog yake www.mvutokwanza.blogspot.com. Mastaa wengine na watanzania igeni mfano wa Wema kusapoti wabunifu wa ndani. Look at the Princess Wema Sepetu...,,
 


0 comments: